Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:24

Majeshi ya Libya yateka miji inayoshikiliwa na waasi


Wapiganaji wa waasi wakijitayarisha kwa mashambulio mbele ya kampuni ya kusafisha mafuta katika mji wa mashariki wa Ras Lanouf , Libya.
Wapiganaji wa waasi wakijitayarisha kwa mashambulio mbele ya kampuni ya kusafisha mafuta katika mji wa mashariki wa Ras Lanouf , Libya.

Vikosi vitiifu na kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi vinaonekana kupata ushindi kwa kuteka baadhi ya miji iliyokua mikononi mwa waasi

Majeshi matiifu na kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi yamewafurusha waasi kutoka mji wa bandari wa mafuta wa Ras Lanuf siku ya Alhamisi. Mashahidi wanasema waasi waliingia katika magari wakipakiza silaha chache walokuwa nazo na kukimbia kutoka mji huo, walipokuwa wanashambuliwa na miziznga kutoka majeshi ya serikali.

Ripoti nyingine zinaeleza kwamba waasi wako katika mapigano makali na majeshi ya serikali katika mji mwengine wa karibu wa Brega.

Wakati huo huo majeshi ya serikali yanadai ushindi wa kunyakuwa Zawiya, mji ulo karibu zaidi na mji mkuu Tripoli ulokuwa umechukuliwa na waasi. Maafisa wa serikali waliripoti Jumatano usiku kwamba majeshi yaliuteka tena mji huo.

Saif al-Islam, kijana wa Gadhafi anasema serikali ya Libya haito kubali kamwe kujisalimisha kwa waasi. Amesema wananchi wa Libya hawato wakaribisha majeshi ya NATO au ya Marekani.

Wakati mapigano yakiendelea, wahamiaji kutoka mataifa mbali mbali wanakimbilia nchi jirani za Libya, hasa Misri na Tunisia.

Afisa habari wa shirika la kaimataifa la uhamiaji IMO, Jumbe Omari Jumbe, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba idadi ya watu wanaovuka mpaka imepungua lakini haimanishi kwamba hakutakuwa na wakimbizi zaidi.

Anasema, "jinsi hali ilivyo na mapigano yanavyoendelea upande wowote utakaopata ushindi utasababisha wafuasi wa wale waloshindwa kukimbia nchi na hivyo tunajitayarisha kupokea wimbi la wakimbizi kutoka Libya".

Siku ya Alhamisi wahamiaji walofika kwenye mpaka kati ya Libya na Tunisia na Libya waliandamana kudai chakula na huduma bora zaidi.

XS
SM
MD
LG