Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:42

Ban Ki Moon alaani ukandamizaji Libya


Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema amekasirishwa sana na ukandamizaji na mashambulio yanayosababisha vifo dhidi ya waandamanaji.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema amekasirishwa sana na ukandamizaji na mashambulio yanayosababisha vifo dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikaliya Libya na kumwambia kiongozi wa nchi hiyo Moammar Gadhafi kusitisha mara moja ghasia hizo.

Bw. Ban alisema alizunguimza na Bw. Gadhafi kwa dakika 40 kwa simu mapema Jumatatu na kumhimiza kwa nguvu kiongozi huyo kusitisha mashambulizi dhidi ya waandamanaji na majeshi ya usalama.

Kwa upande wake kiongozi wa Libya Ghadafi akilihutubia taifa Jumanne alisema wapinzani wa serikali hawawezi kumlazimisha kuacha madaraka na anatarajia kufariki kama shujaa nchini Libya.

Hiyo ilikua hotuba yake ya kwanza ndefu tangu kuanza wimbi la upinzani nchini mwake. Alijieleza kuwa ni mwanamapinduzi, na akawahimiza wafuasi wake kusaidia kuilinda Libya kutokana na wanaochochea ghasia, watu aliyewaeleza kuwa ni magaidi au magengi.

Akizungumza na Sauti ya Amerika mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Abubakar Famau, ambaye ameishi kwa miaka kadhaa huko Libya anasema si jambo la kushangaza kwa maandamano hayo kuanza Bengazi kwa sababu, ni kitovu cha upinzani nchini Libya.

Anasema huenda ikawa rahisi kwa upinzani kuchukua udhibiti wa maeneo mengine ya nchi lakini kwa Tripoli anasema “itabidi kwa waandamanaji kufanya kazi ya ziada mpaka wafanikiwe kupata mji wa Tripoli kwa sababu Tripoli ndio kitovu cha serikali ya Libya na ni mji mkubwa kabisa, na sehemu kubwa ya Libya ni Jangwa.”

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York linakutana kwa faragha kujadili hali ya Libya.

XS
SM
MD
LG