Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:12

Kenya yapokea raia wake kutoka Libya


Wafuasi wa Gadhafi huko Sabratha, kilomita 75 magharibi ya Tripoli.
Wafuasi wa Gadhafi huko Sabratha, kilomita 75 magharibi ya Tripoli.

Raia wa Kenya kutoka Libya waliwasili Nairobi Jumatatu wakisema wametaabika na hata kupigwa kabla ya kuondoka

Raia 90 wa Kenya pamoja na raia wengine kadhaa wa nchi za Afrika Mashariki waliokuwa wakifanya kazi Libya waliwasili Nairobi Jumatatu kutoka Tripoli kufuatia ghasia na michafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo.

Hatua hii inafuatia juhudi za serikali ya Kenya na shirika la ndege la Kenya Airways, kuwaondoa raia wake ili kuwaokoa kutokana na ghasia zinazoendelea nchini Libya. Ndege ya Kenya Airways, ilikuwa imebeba abiria 351 wakiwemo raia kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Lesotho, Zimbabwe na Sudan Kusini.

Taarifa zinasema kulikuwa na zaidi ya raia elfu 30 hadi elfu 40, kutoka nchi tofauti barani humo, waliokuwa katika uwanja wa ndege wa Tripoli wakitafuta msaada wa kuondoka nchini Libya ili kuepuka michafuko ya kisiasa yaliyoanza mwanzoni mwa mwezi huu, lakini baadhi hawakufanikiwa.

Michafuko haya yanafuatia hatua ya waandamanaji wanaoipinga serikali ya Libya wakitaka kiongozi wa nchi hiyo, Kanali Muammar Ghadafi, ajiuzulu baada ya kuwepo madarakani kwa zaidi ya miongo minne.

XS
SM
MD
LG