Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:06

UN yaeleza maji yanarudisha nyuma malengo endelevu ya maendeleo yaliofikiwa


Mkazi wa kitongoji cha Mathare Nairobi, Kenya, March 22, 2023.
Mkazi wa kitongoji cha Mathare Nairobi, Kenya, March 22, 2023.

Leo ni Siku ya Maji Duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu ‘harakisheni mabadiliko.’ Mwezi Oktoba 2022, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa agizo la dharura hatua ichukuliwe kuharakisha maendeleo yanafikiwa ili kuhakikisha upatikanaji wa maji salama kwa wote.

“Kufeli katika mzunguko wote wa maji unarudisha nyuma hatua zote zilizopigwa katika masuala makuu ya kimataifa, kuanzia afya hadi njaa, usawa wa jinsia katika kazi, elimu hadi viwandani, maafa hadi amani,” UN imeeleza.

Kwa mujibu wa ripoti ya UN hivi sasa “tuko nje kabisa ya mwelekeo. Mabilioni ya watu na shule nyingi, biashara, vituo vya afya, mashamba na viwanda vimerejeshwa nyuma kwa sababu haki yao ya kibinadamu kuwa na maji salama na vyoo havijakamilishwa. “Tunahitaji kuharakisha mabadiliko hayo…”

Mtu mmoja kati ya watu wanne katika ulimwengu wetu hana njia ya uhakika kuweza kusimamia maji salama ya kunywa.

Maradhi yanayosababishwa na maji yanaendelea kuwa ni sababu kuu ya vifo, ikikadiriwa kuwa watu 829,000 wanafariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuharisha yanayotokana na maji.

Carmelo Del Valle na binti yake waliolazimika kuhama makazi yao kutokana na mafuriko ya Mto Paraguay, wakiteka maji huko Asuncion, Paraguay, March 18, 2023.
Carmelo Del Valle na binti yake waliolazimika kuhama makazi yao kutokana na mafuriko ya Mto Paraguay, wakiteka maji huko Asuncion, Paraguay, March 18, 2023.

Mkutano wa UN 2023 kuhusu maji

UN inaeleza kuwa bila shaka, 2023 ni mwaka maalum kwa kutekeleza ahadi zinazohusu matumizi ya maji na vyoo.

Maadhimisho haya ya Siku ya Maji Duniani yanafanyika sambamba na kuanza kwa Kongamano la UN 2023 kuhusu Maji (March 22-24, New York).

Kongamano hili ni fursa ya mara moja katika kizazi kuiunganisha dunia kutatua mgogoro wa maji na vyoo.

Serikali za kitaifa na wadau kutoka ngazi zote za kijamii watashirikiana kutoa maoni yao binafsi kuharakisha kufikiwa kwa malengo SDG 6 na malengo mengine yaliyokubaliwa kimataifa yanayohusiana na maji.

Mtu akibeba maji kutoka maji yanayopatikana Caracas, Venezuela Jumatatu, Machi 20, 2023.
Mtu akibeba maji kutoka maji yanayopatikana Caracas, Venezuela Jumatatu, Machi 20, 2023.

Huko nyuma mwaka 2015, dunia ilichukua ahadi ya Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDG) 6 ikiwa ni sehemu ya ajenda ya 2030 – ahadi ya kuwa kila mtu angekuwa anasimamia maji kwa usalama na usafi wa vyoo ifikapo 2030.

Chanzo cha habari hii ni Ripoti ya Umoja wa Mataifa na Ripoti ya Taasisi ya Pure Water for the World.

XS
SM
MD
LG