Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:25

Ukame huenda ukasababisha vifo 135 kwa siku nchini Somalia - UN


Hali ya ukame nchini Somalia.
Hali ya ukame nchini Somalia.

Ukame ulioweka rekodi unaokumba eneo la pembe ya Afrika unaweza kusababisha vifo 135 kwa siku nchini Somalia kati ya mwezi Januari na Juni mwaka huu, wizara ya afya, Shirika la Afya Duniani WHO, na UNICEF zilisema katika ripoti ya utafiti iliyotolewa Jumatatu.

Mapema mwezi Machi, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilionya kuwa karibu watu 100,000 katika nchi hiyo dhaifu wanakabiliwa na viwango vya juu vya janga la njaa kutokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kukumba eneo hilo katika miongo minne.

Utafiti ambao matokeo yake yalitolewa Jumatatu ulitumia vigezo vya takwimu kukadiria kuwa hadi Wasomali 135 wanaweza kupoteza maisha yao kutokana na sababu zinazohusiana na ukame kila siku katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, huku jumla ya vifo vikikadiriwa kuwa kati ya 18,100 na 34,200.

Pia ilisema kuwa hali mbaya ya hewa huenda ilisababisha vifo vya watu 43,000 mwaka jana ikilinganishwa na ukame wa 2017, huku watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wakiwa nusu ya waathiriwa.

"Tunashindana na wakati ili kuzuia vifo na kuokoa maisha", alisema Mamunur Rahman Malik, mwakilishi wa WHO nchini Somalia.

"Gharama ya kutochukua hatua kwetu itamaanisha kuwa watoto, wanawake na watu wengine walio katika mazingira magumu watalipa na maisha yao huku tukiwa hatuna matumaini, tukishuhudia janga hilo likiendelea,” aliongeza.

XS
SM
MD
LG