Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 01:07
VOA Direct Packages

Somalia yapitisha sheria muhimu ya kupambana na kutokomeza ugaidi


Eneo la shambulizi la kigaidi la Somalia. Picha ya maktaba.

Baraza kuu la bunge nchini  Somalia Jumatano limeidhinisha sheria muhimu dhidi ya ugaidi ambayo inalenga kuweka  muundo wa kisheria ambao utasaidia idara za usalama za serikali kupambana vyema na kutokomeza ugaidi nchini humo.

Wabunge wameidhinisha mswaada huo kwa kura 133 dhidi 3, wakati 7 wakijiweka kando katika upigaji kura, baada ya wiki kadhaa za majadiliano katika kile ambacho mkuruguenzi wa upelelezi wa Somalia, Mahad Mohamed Salad ameita ni sheria muhimu ili kuifanya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kuwa mahala salama.

Hata hivyo wakosoaji wa sheria hiyo wanasema kwamba ni pana mno katika ufafanuzi wa nani ni gaidi, na hivyo kuonya kwamba huenda ikatumiwa vibaya na idara za usalama za serikali. Mohamed Ibrahim Moalimuu ambaye alikuwa mwanahabari na sasa ni mbunge, aliyenusurika mashambulizi ya kigaidi ya al Shabab mara 5, amesema kwamba sheria hiyo haitakiwi kutumiwa na idara za serikali kukamata watu kirahisi bila ya idhini ya mahakama.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG