Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:33

Ukraine inajiandaa kwa mashambulizi zaidi Siku ya Maadhimisho ya Uhuru


Bendera kubwa ya Ukrainian yatandazwa wakati wa siku ya sherehe za Uhuru wa Ukraine huko katika kasri ya kihistoria mjini Brussels, August 24, 2022.
Bendera kubwa ya Ukrainian yatandazwa wakati wa siku ya sherehe za Uhuru wa Ukraine huko katika kasri ya kihistoria mjini Brussels, August 24, 2022.

Wananchi wa Ukraine Jumatano wameadhimisha miaka 31 tangu kujitenga na Umoja wa Soviet iliyokuwa chini ya Russia katika kile kiko wazi kuwa ni siku ya huzuni, lakini maadhimisho yaliendelea huku  yakiwa yamegubikwa na hofu ya Russia kufanya mashambulizi mapya ya makombora.

Zelenskyy asema Russia imeshindwa kuwanyang'anya wananchi wa Ukraine uhuru wao
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:01 0:00

Siku ya Uhuru ya Ukraine, ambayo imeangukia miezi sita baada ya uvamizi wa Russia Februari 24, mwaka huu imechukua umuhimu wenye utakatifu kwa Waukraine ambao wamepania kutoangukia tena kwenye utawala wa Moscow.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameonya siku ya Jumanne jioni juu ya uwezekano wa “mashambulizi ya kiuchokozi yasiokubalik ya Russia” na mashambulizi ya kinyama” yanayofanywa na Moscow kufunika ile alichosema ilikuwa ni siku muhimu kwa Waukraine wote.

Rais Zelensky akihutubia Jumuiya ya Wanateknolojia wa kimataifa kutoka Kyiv, Ukraine.
Rais Zelensky akihutubia Jumuiya ya Wanateknolojia wa kimataifa kutoka Kyiv, Ukraine.

Maafisa wamepiga marufuku mikusanyiko ya umma katika mji mkuu Kyiv na imeweka amri kali ya kutotoka nje usiku upande wa mashariki mwa mji wa Kharkiv, ambao umeharibiwa kufuatia mashambulizi yaliyodumu kwa miezi kadhaa katika mstari wa mbele.

Ukraine ilijitenga na Umoja wa Soviet mwezi Agosti 1991 baada ya jaribio la mapinduzi ya ghasia kushindwa mjini Moscow na wananchi wa Ukraine kwa idadi walipiga kura ya maoni kutangaza uhuru wao.

Zelenskyy hajaeleza kwa kina jinsi serikali itakavyo adhimisha sikukuu hiyo ya umma, kwa sababu za kiusalama. Amesema atakuwa akiwatunukia zawadi watu, kama vile wafanyakazi wa huduma za reli, huduma za dharura, wahandisi wa umeme, madereva, wasanii na wale walioko katika vyombo vya habari.

XS
SM
MD
LG