Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:54

Uhusiano wa Uturuki na Russia waendelea kuimarika


Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan kwenye picha ya awali alipokutana na rais wa Russia Vladimir Putin

Meli mbili zaidi Jumatatu zimeondoka Ukraine zikielekea Ugiriki na Misri zikiwa zimebeba tani elfu 30 za nafaka. 

Tangu Uturuki kuongoza makubaliano kati ya Russia na Ukraine mwezi Julai ya kuruhusu usafirishaji wa nafaka, tayari zaidi ya tani 600,000 za bidhaa hizo zimesafirishwa kutoka kwenye bandari za Ukraine. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akifuatana na rais wa Utruruki Recep Tayyip Erdogan hivi karibuni wamekitembelea kituo kinachoratibu usafishaji huo mjini Istanbul.

Wakati akizungumza mbele ya wanahabari, Guterres ameelezea umuhimu wa makubaliano hayo. Guterres amesema kwamba Utruruki ilikuwa mstari wa mbele katika kufanikisha makubaliano hayo. Kutokana na wingi wa meli zinazoondoka kwenye bandari za Ukraine, Uturuki ina kila sababu ya kuendelea kuwa na uhusiano wa karibu na Russia.

Edorgan anasema kwamba kwa kudumisha uhusiano wa karibu na Putin pamoja na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ambaye alikutana naye wiki iliyopita nchini mwake, yeye yupo katika nafasi bora zaidi ya kuyashawishi mataifa hayo kusitisha mapigano. Kufikia sasa mataifa ya magharibi hayajalalamika moja kwa moja kuhusu uhusiano wa karibu kati ya Edorgan na Putin, labda pengine kutokana na kwamba ushirikiano huo umesaidia katika kupunguza tatizo la chakula ulimwenguni ,lililosababishwa na mzozo wa Ukraine.

XS
SM
MD
LG