Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 21:29

Mji ulio karibu na kinu cha nyuklia cha Ukraine washambuliwa kwa makombora


Picha inayoonyesha kinu cha nyuklia cha Ukraine cha Zaporizhzhia. Picha ya Reuters
Picha inayoonyesha kinu cha nyuklia cha Ukraine cha Zaporizhzhia. Picha ya Reuters

Mji wa kusini mwa Ukraine wa Nikopol ambao hauko mbali na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia umeshambuliwa kwa makombora mapema Jumapili, huku rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akionya kwamba Russia huenda ikajaribu kufanya kitendo kibaya cha ukatili wiki hii.

Russia ililenga maeneo yaliyo karibu na Odesa, bandari kubwa ya Ukraine kwenye bahari ya Black Sea na kitovu cha usafirishaji wa nafaka.

Lakini mashambulizi ya mabomu dhidi ya mji wa Nikopol yamesababisha hofu kubwa, huku gavana wa jimbo la Ukraine Valentyn Reznichenko akiandika kwenye app ya ujumbe wa Telegram kwamba mji huo ulishambuliwa na makombora 25, na kusababisha moto kwenye kituo cha viwanda na kukata umeme kwa watu 3,000.

Uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine utatizima miezi sita Jumatano ambapo itakuwa siku ya maadhimisho ya uhuru wa Ukraine.

Rais Zelensky Jumamosi alisema katika ujumbe wake wa kila usiku,” Tunapaswa kufahamu kwamba wiki hii Russia inaweza kujaribu kufanya jambo baya hasa, jambo la kikatili. Huyo ndiye adui yetu. Lakini katika wiki nyingine yoyote katika miezi hii sita, Russia itafanya jambo lile lile wakati wote la kuchukiza na la ukatili.”

XS
SM
MD
LG