Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:29

Russia yadaiwa kufanya mashambulizi mapya kwenye kinu cha nyuklia


Kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia ambcho kinaendeleza mgogoro wa Ukraine na Russia.
Kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia ambcho kinaendeleza mgogoro wa Ukraine na Russia.

Ukraine imeripoti mashambulizi mapya ya anga ya Russia, karibu na kinu kikubwa cha nyuklia.

Hayo yakitokea rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, ametahadharisha kuhusu matendo zaidi ya Russia, huku Ukraine ikijiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru.

Gavana wa kikanda Valentyn Reznichenko, amesema roketi za Russia, zilishambulia eneo la magharibi la kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia.

Roketi zilishambula nyumba, shule ya chekechea na maduka amesema Reznichenko.

Russia na Ukraine, zimekuwa zikilaumiana kwa mashambulizi ya mara kwa mara katika kinu hicho cha nyuklia.

Ukraine imeusihi Umoja wa Mataifa, na mashirika mengine ya kimataifa kuilazimisha Russia, kuondoka katika sehemu hiyo ambayo imekaa hapo toka Machi licha ya kwamba wataalamu wa nyuklia wakifanyakazi katika kinu hicho.

XS
SM
MD
LG