Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 06:19

Ufaransa: Putin atafakari madai yake ya awali wakaguzi wa nyuklia kupitia Russia


Kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia, Ukraine.
Kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia, Ukraine.

Ofisi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ilisema Ijumaa kuwa Rais wa Russia Vladimir Putin “anafikiria tena” madai yake ya awali kwamba wakaguzi wa  Shirika la  Kimataifa la Nishati ya Atomiki wasafiri kupitia Russia.

Wakaguzi hao watakuwa wanaelekea kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine, kinachokaliwa kimabavu na Moscow, mtambo mkubwa sana wa nyuklia barani Ulaya.

Kuna wasiwasi unaoongezeka Ulaya kuwa mashambulizi kuzunguka kituo hicho cha Zaporizhzhia yanaweza kupelekea janga baya sana kuliko lile lililotokea mwaka 1986 katika kinu cha nyuklia cha Chernobyl.

Mkuu wa IAEA Rafael Grossi “amefurahishwa na taarifa za karibuni zilizoashiria kwamba pande zote Ukraine na Russia wanaunga mkono lengo la IAEA kupeleka ujumbe” kwenye kinu hicho.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya kila siku ya Ijumaa, “wanadiplomasia wa Ukraine, washirika wetu, wawakilishi wa UN na wa IAEA wanashughulikia maelezo maalum ya ujumbe huo utakaotumwa katika kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia. … Namshukuru kila mtu ambaye amejiunga kulishughulikia hili na juhudi zao.”

Zelenskyy pia alitahadharisha katika hotuba yake, “Kama usaliti wa Russia juu ya miale hii ya nyuklia utaendelea, kipindi hiki cha joto kinaweza kuingia katika historia ya nchi mbalimbali za Ulaya kuwa ni moja ya majanga mabaya zaidi kuwahi kutokea.

Kwa sababu hakuna agizo hata moja katika kinu chochote cha nishati ya nyuklia ulimwenguni kinaweza kutabiri utaratibu wakufuata iwapo taifa la kigaidi litakigeuza kinu cha nishati ya nyuklia kuwa ndio shabaha yake."

Baadhi ya taarifa ya habari hii inatokana na shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG