Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 09:48

Ukraine yaishtumu Russia kushambulia kiwanda kikubwa cha nyuklia


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy

Ukraine Jumapili imeishtumu kwa mara nyingine Russia kwa kushambulia kwa mabomu kituo kikubwa cha nishati ya nyuklia kinachopatikana katika mji wa Zaporizhzhia, na kudai kwamba Moscow imejihusisha katika “ugaidi wa nyuklia.”

Kiwanda hicho cha nyukilia cha serikali ya Ukraine kimesema wanajeshi wa Russia waliharibu mitambo mitatu ya mionzi kwenye kiwanda hicho katika shambulio la Jumamosi usiku na kujeruhi mfanyakazi mmoja kwa kombora.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameandika kwenye Twitter “Ugaidi wa nyukilia wa Russia unahitaji jibu kali la Jumuia ya Kimataifa, kuweka vikwazo kwenye sekta ya nyuklia ya Russia na mafuta ya nyuklia.”

Kiwanda hicho kilichoko katika eneo linalodhibitiwa na Russia, kilishambuliwa pia siku ya Ijumaa, Moscow iliwashtumu wanajeshi wa Ukraine kwa mashambulizi hayo.

Russia ilikiteka kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia mapema mwezi Machi katika hatua za mwanzo za uvamizi wake dhidi ya Ukraine, lakini kiwanda hicho bado kinaendeshwa na mafundi wa Ukraine.

Baada ya shambulio la kwanza la Ijumaa, shirika la kimataifa la nishati ya Atomic lilisema mashambulizi hayo ya makombora yameonyesha hatari ya janga la nyuklia.

XS
SM
MD
LG