Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 14:50

Ujumbe wa AU waanza uchunguzi wa mauaji ya raia Somalia


FILE - Walinda Amani wa Umoja wa Afrika (AMISOM) mjini Mogadishu, Somalia. Feb. 28, 2019.
FILE - Walinda Amani wa Umoja wa Afrika (AMISOM) mjini Mogadishu, Somalia. Feb. 28, 2019.

Ujumbe wa Walinda Amani wa Umoja wa Afrika , AU, nchini Somalia umesema umeanza uchunguzi wa raia waliouwawa wakati wa mapigano ya silaha baina ya vikosi vyake na kundi la al-Shabaab lenye uhusiano na al-Qaida.

Jeshi linalojulikana kama AMISOM limesema tukio hilo lilitokea Jumanne kufuatia shambulizi la ghafla wakati wanajeshi wake walipokuwa katika doria katika operesheni kwenye kambi ya Beldamin- Golwen katika mkoa wa lower shabel.

Kulikuwa na mapambano makubwa ya silaha kati ya vikosi vya AMISOM na wanamgambo wa al-Shabaab kabla ya kikosi cha doria kukamata silaha, risasi pamoja na simu za mkononi, taarifa imeeleza leo.

Raia saba waliuawa katika tukio hilo mkulima mmoja kutoka kijiji cha Golwen ameliambia shirika la Habari la Reuters leo, akiwemo kaka yake Omar Hassan anayemiliki shamba katika eneo hilo, dereva mmoja na wakulima wengine watano.

Walinda amani wa AU walipelekwa Somalia kwa mara ya kwanza mwaka 2007 kuisaidia serikali dhidi ya kikundi cha al-Shabaab.

XS
SM
MD
LG