Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 10:46

Mlipuko wa bomu waua tisa Mogadishu


Vikosi vya usalama vikiwasili katika mabaki ya geri iliyolipuka mjini Mogadishu, Somalia, July 10, 2021.
Vikosi vya usalama vikiwasili katika mabaki ya geri iliyolipuka mjini Mogadishu, Somalia, July 10, 2021.

Takriban watu tisa wameuawa na tisa wamejeruhiwa Jumamosi katika bomu la kujitoa mhanga lililolenga msafara wa serikali karibu na hospitali mbili kubwa katika mji mkuu w Somalia, Mogadishu.

"Mlipuko mkubwa ulisababisha wingu la moshi angani na kuharibu majengo ya biashara ikiwemo migahawa, niliweza kuona miili ya watu waliokufa takriban watu wanane," Hussein Jim'ale, dereva wa usafiri wa umma ambaye alishuhudia tukio alimueleza mwandishi wa habari katika eneo hilo.

Mlipuko ulitokea karibu na njia panda yenye harakati nyingi kati ya hospitali za Banadir na Madina

Maafisa usalama wamesema mwanamme mmoja aliyekuwa anaendesha gari la kifahari lililojaa vilipuzi aliulenga msafara wa afisa mwandamizi wa polisi, Kanali Farhan Qarole ambaye alinusurika katika shambulizi.

Maafisa wa afya wameiambia VOA Idhaa ya Kisomali kuwa watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali mbili za karibu na kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka.

Lilikuwa ni shambulizi la pili la kigaidi mjini humo mwezi huu. Wiki moja iliyopita, shambulizi la kujitoa mhanga la al-Shabab kwenye mgahawa wa kuuza chai karibu na idara ya upelelezi ya Somalia liliua watu 10 na kujeruhi dazeni. Takriban watu 15 waliuawa na zaidi ya 20 walijeruhiwa mwezi uliopita wakati mlipuaji bomu wa kujitoa mhanga alipotegua milipuko mbele ya kituo cha mafunzo cha serikali mjini Mogadishu.

Wachambuzi wanasema kundi hilo la kigaidi limezidisha mashambulizi yake kabla ya uchaguzi mkuu ujao, ambao unatarajiwa kufanyika ndani ya kipindi cha miezi minne ijayo.

XS
SM
MD
LG