Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 17:00

Upinzani Somaliland wapata ushindi wa kishindo


Wafuasi wa wagombea wa chama cha upinzani Waddani wakiwa katika mkutano wa hadhara wakati wa uchaguzi wa Somaliland huko Hargeisa.
Wafuasi wa wagombea wa chama cha upinzani Waddani wakiwa katika mkutano wa hadhara wakati wa uchaguzi wa Somaliland huko Hargeisa.

Vyama viwili vya upinzani vya Jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland, kwenye Pembe mwa Afrika, vimepata ushindi wa viti vingi vya bunge kwenye uchaguzi wa wiki iliyopita.

Tume ya uchaguzi ya jimbo hilo ilitangaza Jumatatu kwamba chama cha Waddani kimepata viti 31 na kile cha Ucid kilipata viti 21.

Chama tawala cha Kulmiye kimepata viti 30 kwenye bunge lenye viti 82.

Kwa upande mwengine hakuna mwanamke hata mmoja aliyegombania kiti cha bunge aliyeweza kupata ushindi katika uchaguzi huo.

Jamhuri hiyo iliyokuwa sehemu ya Somalia ilijitangazia uhuru mwaka 1991 na haijatambuliwa kimataifa hadi hii leo.

Hata hivyo serikali hiyo imefanikiwa kufanya uchaguzi mara kadhaa chini ya mfumo wa kidemokrasia.

XS
SM
MD
LG