Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:03

Uchaguzi wa Somalia waanza kwenye baadhi ya sehemu


Wabunge wa Somalia wainua mikono kwenye uchaguzi wa awali .
Wabunge wa Somalia wainua mikono kwenye uchaguzi wa awali .

Zoezi la kupiga kura lilianza Alhamis katika moja ya majimbo ya Somalia likiwa limechelewa kwa siku kadhaa, lakini limefanyika kabla ya nchi nzima ambapo awamu ya kwanza ya uchaguzi wa kitaifa, haijaweza hata kuanza.

Uchaguzi wa bunge na rais uliosuburiwa kwa muda mrefu ulitarajiwa kuanza tarehe 25 Julai, kulingana na ratiba ilioafikiwa na viongozi wa kisiasa baada ya miezi kadhaa ya mivutano mikali juu ya mchakato huo.

Uchaguzi nchini Somalia unafuata mfumo wakutatanisha wa uchaguzi siyo wa moja kwa moja, na katika hatua ya kwanza ya upigaji kura, majimbo matano yanatakiwa kuwachagua maseneta wa baraza la seneti katika bunge la taifa.

Lakini hakuna hata jimbo moja lililokuwa tayari, na hakuna hata jimbo moja lililopiga kura tarehe iliowekwa, na hivyo kuisambaratisha ratiba ya uchaguzi.

Jubaland, jimbo linalopakana na Kenya ambalo lilikuwa limejianda vya kutosha, lilipiga kura Alhamisi, na kuwachagua wagombea wanne kwenye baraza la seneti lenye maseneta 54.

Rais wa jimbo hilo Ahmed Madobe ameipongeza Jubaland kwa kuanzisha uchaguzi wa muda mrefu uliocheleweshwa mara kadhaa.

XS
SM
MD
LG