Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 17:37

Uingereza kuanza kuwachoma watoto wa miaka 16-17 chanjo ya COVID-19


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Watoto wote nchini Uingereza wenye miaka 16 na 17, watastahiki kuchomwa dozi ya kwanza ya chanjo ya COVID-19 ifikapo Agosti 23, Huduma ya Taifa ya Afya ilitangaza leo Jumapili.

Kupatiwa chanjo ifikapo tarehe ya mwisho katika mwezi wa Agosti, kutawawezesha vijana waliopo kwenye umri huo, kupata wiki mbili zinazohitajika kwa chanjo ili kuongeza kinga muhimu mwilini, wizara ya afya ilisema.

Waziri wa Afya na Huduma za jamii, Sajid Javad alisema katika taarifa, kwamba kupata chanjo ifikapo Agosti 23, kutahakikisha kwamba vijana wanapata kinga muhimu wanayoihitaji kabla ya kurudi shuleni mwezi Septemba.

Program mpya imezinduliwa, kuwasaidia vijana kutafuta kituo cha chanjo kilicho karibu nao, na kufika bila kuweka miadi. Maelfu ya vijana katika umri huo, tayari wamepatiwa dozi za chanjo, wizara ya afya ilisema.

XS
SM
MD
LG