Hata hivyo wanaoingia nchini lazima wapimwe corona kabla ya kuingia ndege, na pia wapimwe tena siku mbili baada ya kuingia nchini humo, japo sasa hawatawekwa kwenye karantini kama ilivyokuwa hapo awali.
Watu kutoka Ufaransa hata hivyo wataendelea kuwekwa kwenye karantini baada ya kuwasili Uingereza kutoka na idadi kubwa ya maambukizi ya aina mpya ya virusi vya beta nchini humo, vilivyo gunduliwa kwa mara ya kwanza Afrika kusini.
Uingereza ni mojawapo ya mataifa yanayoongoza katika utoaji wa chanjo za covid ikisemekana kuwa karibu asilimia 90 ya watu wazima nchini humo tayari wamepokea walau chanjo ya kwanza. Taifa hilo limepanga kuanza kutoa chanjo ya tatu maarufu kama booster, kwa wakazi wake milioni 32 hapo mwezi Septemba.