Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:56

Kemri kupokea mfumo wa Uingereza kusaidia utafiti wa COVID-19


FILE - Afisa wa Afya akichukua sampuli ya COVID-19 katika maabara ya Taasisi ya Utafiti ya Afya (KEMRI) huko Kisumu, magharibi Kenya, Apr. 23, 2020.
FILE - Afisa wa Afya akichukua sampuli ya COVID-19 katika maabara ya Taasisi ya Utafiti ya Afya (KEMRI) huko Kisumu, magharibi Kenya, Apr. 23, 2020.

Taasisi ya utafiti wa tiba nchini Kenya, Kemri, itaweza kupokea na kutumia mfumo wa kipekee wa Uingereza kufanya utafiti kuhusiana na virusi vya corona.

Kupitia mpango wa mfumo huo wa kuchunguza aina mbali mbali ya virusi vipya, Kemri itaweza kutumia vifaa na kemikali za Uingereza ili kuongeza uwezo wa nchi kuchunguza, kupata ushauri wa kifundi na mafunzo.

Balozi wa Uingereza nchini Kenya Jane Marriot alisema ushirikiano huo utaimarisha uhusiano kati ya nchi zao mbili.

Waziri wa Afya wa Kenya Muthai Kagwe alifurahia ushirikiano huo ambao alitia saini pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza Dominic Raab mwezi Januari.

XS
SM
MD
LG