Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:37

COVID-19 : Johnson na Sunak watajitenga baada ya kukaribiana na maambukizi


Waziri Mkuu Boris Johnson na Waziri wa Fedha Rishi Sunak
Waziri Mkuu Boris Johnson na Waziri wa Fedha Rishi Sunak

Huduma ya taifa ya afya nchini Uingereza imewasiliana na Waziri Mkuu Boris Johnson na Waziri wake wa fedha, Rishi Sunak, kuwafahamisha walikaribiana na mtu ambaye alipimwa na kugundulika ana COVID-19.

Downing Street, Imesema Jumapili katika taarifa yake kuwa, viongozi hao watashiriki katika majaribio ya kila siku ya upimaji, ambayo yatawaruhusu kuendelea kufanya kazi katika majengo ya Downing Street, lakini wajitenge wakati hawapo katika ofisi zao.

Tangazo hilo limekuja baada ya Waziri wa Afya wa Uingereza, Sajid Javid, ambaye anaongoza kitengo cha majibu kuhusu virusi vya Corona nchini humo, alisema jana Jumamosi, yeye amepimwa na kukutwa ana COVID-19.

Hivi sasa amesema tayarina anajitenga ili kuzuia virusi kusambaa kwa wengine.

Wakati huo huo, kesi za COVID-19 zinaongezeka nchini Marekani na duniani kote, kwa kiasi kikubwa zinatokana na aina mpya ya virusi vya Corona vya delta.

Maeneo yanaanza kurejesha masharti kama vile kuvaa barakoa ili kupunguza idadi ya waathirika.

XS
SM
MD
LG