Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 07:15

Biden ajadili mahusiano imara na Canada, Mexico na Uingereza


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson akiongea kwa simu na Rais Joe Biden kutoka London.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameweka bayana kwa Rais Joe Biden Jumamosi kuwa ana nia ya kuanzisha makubaliano mapya ya kibiashara kati ya Marekani na Uingereza.

Hatua ya msukumo huo wa Johnson kufikia makubaliano imekuja wakati wa mazungumzo mapana kati ya viongozi hao yaliyo gusia ulimwengu kukabiliana na janga la virusi vya Corona na tangazo la uongozi wa Biden wiki hii kuwa Marekani itajiunga tena na mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris na Shirika la Afya Duniani, kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya Johnson ya Downing Street.

Mkataba mpya wa kibiashara kati ya washirika ni kipaumbele cha juu kwa Johnson kuliko Biden. Uingereza imepata tena udhibiti wa sera yake ya taifa ya biashara mwanzoni mwa mwezi Januari baada ya kumalizika kipindi cha mpito cha Brexit.

Msemaji wa White House Jen Psaki alisema Ijumaa uongozi haukuwa na muda maalum wa kuanzisha makubaliano mapya ya kibiashara kwa sababu Biden yuko makini kwa kiasi kikubwa kuangazia kudhibiti janga la virusi vya corona na kushinikiza Bunge kupitisha mpango wa afueni wa athari za virusi vya corona wa dola trilioni 1.9.

Maongezi yake na Johnson ni takriban ya tatu ambayo Biden amefanya na viongozi wenzake tangu Ijumaa. Rais alizungumza pia na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador Ijumaa jioni.

Msaada wa kudhibiti uhamiaji

Siku ya Jumamosi, Lopez Obrador alisema Biden amemwambia kuwa Marekani itapeleka dola bilioni 4 kusaidia maendeleo Honduras, El Salvador na Guatemala, mataifa ambayo ugumu wa maisha umesukuma wimbi la wahamiaji kupitia Mexico wanaoelekea Marekani.

Lopez Obrador alisema wakati wa mazungumzo yao Ijumaa, walijadili uhamiaji na kutafuta ufumbuzi wa kiini cha watu kwa nini wanataka kuhama. Mexico imezuia jaribio la hivi karibuni la msafara wa wahamiaji kutoka Amerika ya Kati kuvuka mpaka kuingia Mexico.

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador
Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador

Mazungumzo ya Biden kwa sim una Lopez Obrador yamekuja wakati kuna mvutano, siku kadhaa baada ya rais wa Mexico kuutuhumu Uongozi wa Usimamizi wa Kuzuia Dawa wa Marekani kwa kuzua tuhuma za usafirishaji wa dawa dhidi ya waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi hiyo.

Lakini Lopez Obrador alisema katika taarifa yake ya Ijumaa kuwa mazungumzo yake na Biden yalikuwa ya “kuheshimiana na kirafiki.”

Mazungumzo ya Biden na Trudeau yamekuja baada ya waziri mkuu wa Canada wiki hii kuelezea masikitiko yake kwa umma juu ya uamuzi wa Biden kutangaza amri ya kiutendaji ya kusimamisha ujenzi wa bomba la mafuta la Keystone XL.

Mradi huo wenye utata wa muda mrefu ulikuwa unakadiriwa utasafirisha kiasi cha mapipa 800,000 ya mafuta kwa siku kutoka tar sands huko Alberta hadi pwani ya Ghuba ya Texas, ikipitia Montana, South Dakota, Nebraska, Kansas na Oklahoma.

Biden alimwambia Trudeau kuwa kutangaza kwake amri hiyo alikuwa anatekeleza ahadi ya kampeni yake, afisa mwandamizi wa serikali ya Canada ameliambia shirika la habari la Assoicated Press. Afisa huyo aliongea kwa sharti asitajwe jina lake kujadili mazungumzo hayo binafsi.

White House imesema katika taarifa yake kuwa Biden amekiri masikitiko ya Trudeau na uamuzi huo alioufanya Biden katika mradi wa Keystone.

Ni nadra kawa na makubaliano kamili

Trudeau amewaambia waandishi kabla ya mazungumzo yake Ijumaa na Biden kuwa hataruhusu tofauti zake na Biden juu ya mradi huo kuwa ni chanzo cha mvutano katika uhusiano wa Marekani na Canada.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau

Biden na Trudeau pia wamejadili uwezekano wa Canada kupatiwa chanjo za COVID-19 kutoka kampuni kubwa ya dawa ya Pfizer huko Kalamazoo, Michigan, kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa ngazi ya pili wa serikali ya Canada, aliyeongea kwa sharti asitajwe jina katika kueleza mazungumzo hayo binafsi.

Canada ilikuwa inapata dozi zake za chanjo aina ya Pfizer kutoka kiwanda cha Pfizer kilichoko Puurs, Ubelgiji, lakini Pfizer imeifahamisha Canada haitaweza kupokea dozi zozote wiki ijayo na itapata asilimia 50 pungufu kuliko ilivyokuwa awali katika wiki tatu zijazo.

Ontario Premeir Doug Ford imemuomba wazi wazi Biden kushirikiana dozi milioni moja zinazo tengenezwa katika kiwanda cha Pfizer kilichoko Michigan.

Serikali kuu ya Marekani ina mkataba na Pfizer ambapo dozi za kwanza milioni 100 za chanjo zinazo zalishwa Marekani zitamilikiwa na serikali ya Marekani na kugawanywa ndani ya Marekani.

Viongozi hao wawili pia wamezungumzia kwa upana masuala ya biashara, ulinzi na mabadiliko ya hali ya hewa. Trudeau pia aliibua kesi za wananchi wawili wa Canada waliofungwa nchini China kwa kile kinachoonekana ni ulipizaji kisasi kufuatia kukamatwa kwa mtendaji wa juu wa kampuni ya Huawei, aliyekamatwa Canada kwa ombi la Marekani likiitaka Canada iwakabidhi, kwa mujibu wa ofisi ya waziri mkuu.

XS
SM
MD
LG