Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 15:04

Baraza la Seneti lamuidhinisha WazIri wa Ulinzi


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin

Rais wa Marekani Joe Biden alipata msukumo Ijumaa kwa wabunge kumuidhinisha waziri wake wa Ulinzi, ambaye anakuwa ni wapili katika Baraza la Mawaziri kuthibitishwa wakati uongozi huo ukiendelea kupambana dhidi ya maadui wakuu.

Baraza la Seneti lilipiga kura 93-2 kumthibitisha Jenerali mstaafu Lloyd Austin, anakuwa Mmarekani Mweusi wa kwanza kuongoza Wizara ya Ulinzi.

Baraza la Seneti
Baraza la Seneti

Austin hakupoteza muda kuanza kazi, alipowasili Wizara ya Ulinzi saa moja baadae kuapishwa kuanza kazi, alipokea muhtasari wa taarifa za kijasusi na kukutana na mwenyekiti wa Muungano wa Wakuu wa Wafanyakazi na maafisa wa waandamizi wa jeshi la ulinzi.

Pia alitarajiwa kuongea kwa simu na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg na kupewa muhtasari wa taarifa za operesheni zinazoendelea China na Mashariki ya Kati.

Katika ujumbe wake kwa majeshi ya Marekani, Austin alisema kipaumbele chake cha kwanza kama waziri wa ulinzi angeboresha juhudi za taifa hili “kudhibiti” janga la virusi vya corona.

“Sisi lazima tuisaidie serikali kuu kusonga mbele na kwa haraka kuondoa athari za mbaya zinazotokana na virusi vya corona,” aliandika, akipongeza kazi ambayo tayari imefanywa na jeshi la Marekani.

Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin, kulia, akisalimiana na mkuu wa muungano wa viongozi wa jeshi Mark Milley alipowasili Pentagon, Ijumaa, Jan. 22, 2021, Washington. (AP Photo/Alex Brandon)
Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin, kulia, akisalimiana na mkuu wa muungano wa viongozi wa jeshi Mark Milley alipowasili Pentagon, Ijumaa, Jan. 22, 2021, Washington. (AP Photo/Alex Brandon)

Austin pia ameahidi kuhakikisha kuwa wanajeshi “wana vitendea kazi, teknolojia, silaha na mafunzo kuzuia na kuwashinda maadui wetu.”

“Ina maanisha kuweka sera imara na mikakati na kuwawekea mipango isiyotatanisha,” aliandika, akiongeza kunahaja pia “kuweka umuhimu katika ushirikiano na washirika wetu na wadau wetu.”

Kura ya Baraza la Seneti kumthibitisha Austin ilipigwa chini ya saa 24 baada ya Baraza la Seneti na Baraza la Wawakilishi kupitisha sheria iliyo takiwa kuondoa kikwazo kwa Austin, kamanda wa zamani wa majeshi ya Marekani huko Mashariki ya Kati na Asia Kusini, kushika wadhifa wa kiraia kabla ya miaka saba kupita baada ya kustaafu jeshini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG