Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 04:55

Maseneta waDemocratic wanataka Cruz na Hawley wachunguzwe na kamati ya maadili


Seneta Ted Cruz

Maseneta hao wanasema Ted Cruz na Josh Hawley walijua madai ya udanganyifu katika upigaji kura hayakuwa na msingi na yalipelekea vitisho na vurugu wakati wabunge wanapiga kura ya kumuidhinisha rasmi Biden kama mshindi wa uchaguzi wa urais Marekani

Maseneta saba wa chama cha Democratic wanaiomba kamati ya sheria katika baraza la seneti la Marekani kuwachunguza maseneta wa Republican, Ted Cruz na Josh Hawley kufahamu kikamilifu jukumu lao katika uasi uliofanywa Januari 6 mwaka huu katika jengo la bunge la Marekani na wafuasi wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Maelfu ya wafuasi walikusanyika siku hiyo wakati bunge la Marekani lilipokuwa linapiga kura kumuidhinisha rasmi Joe Biden kama mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 3 mwaka 2020 dhidi ya Trump wakati Hawley na Cruz waliongoza pingamizi katika seneti kutokubali ushindi wa Biden.

Seneta Josh Hawley
Seneta Josh Hawley

Maseneta wa Democratic wanasema Cruz na Hawley walijua madai ya udanganyifu katika upigaji kura hayakuwa na msingi, na yalipelekea vitisho na vurugu. Wa-Democratic wanasema vitendo hivyo vilisababisha waasi kuona wapo sahihi na kupanga vurugu zilizopelekea kuingia ndani ya jengo la bunge. Cruz na Hawley wamelaani vurugu hizo za Januari 6.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG