Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 22:11

Mtangazaji mashuhuri Larry King afariki


Mtangaaji mashuhuri wa Marekani Larry King aliyeaga dunia tarehe 23 Janauari, 2021.
Mtangaaji mashuhuri wa Marekani Larry King aliyeaga dunia tarehe 23 Janauari, 2021.

Mtangazaji wa miaka mingi wa Marekani Larry King ambaye alipata umaarufu mkubwa kwa kipindi chake cha televisheni cha Larry King Live, aliaga dunia Jumamosi akiwa na umri wa miaka 87.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni ambayo alikuwa mmoja wa waanzilishi, Ora Media Services, King alifariki katika kituo cha Cedars-Sinai mjini Los Angeles ambako alikuwa amelazwa nbaada ya kuugua.

Kwa miaka 63, mwanahabari huyo tajika alitangaza kwa redio na televisheni ambapo aliweka rekodi kwenye kitabu cha kumbukumbu cha Guiness World Book of Records kama mwenyeji wa kipindi kilichoendelea kwa muda mrefu zaidi kwa kituo kimoja cha televisheni.

Alijiunga na shirika la habari la CNN Mwaka wa 1985 na kuanzisha kipindi cha "Larry King Live" kilichoendelea kwa miaka 25 hadi alipostaafu.

Katika ujumbe wa rambirambi Jumamosi asubuhi, Rais wa CNN Jeffrey Zucker alisema, "Larry King alichangia pakubwa katika kuliangazia kurunzi shirika hili na kuliweka kwenye ramani ya kimataifa."

King alifanya maelfu ya mahojiano na watu mashuhuri kote duniani wakiwemo marais, mawaziri wakuu, viongozi mbalimbali wa kisiasa na hata wasanii wa tabaka mbalimbali.

Baada ya kustaafu kutoka kwa kituo cha televisheni cha CNN mnamo mwaka wa 2010, alianzisha makala yake "Larry King Now" ambayo yalipeperushwa kwa redio na vituo mbalimbali vya televisheni.

Wachambuzi wanamtaja kama aliyekuwa na ustadi wa kipekee wa utangazaji na aliyefanya mahojiano yake bila kuwashininikiza wageni, na hivyo kuwafanya wajihisi huru na kuzungumza bila kujidhibiti.

Mavazi yake pia yalikuwa ya kipekee kwani kila alipoonekana kwenye televisheni, alivaa saspenda za kuvutia, shati na tai zilizowiana.

Larry alilazwa kenye hospitali ya Cedars -Sinai mapema mwezi Januari, 2021 akiugua ugonjwa wa Covid-19.

-Habari zaidi zitafuata.

XS
SM
MD
LG