Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 22:53

Mitch McConnell anapendekeza kesi dhidi ya Trump icheleweshwe kwa muda


Rais wa zamani Marekani, Donald Trump

Wabunge wa Democratic wanataka kesi isikilizwe haraka wakati Rais Joe Biden anaanza muhula wake wakisema kusomewa mashtaka kamili kwa Trump ni muhimu kabla ya nchi na Congress kusonga mbele

Kiongozi wa Wa-Republican katika baraza la seneti Mitch McConnell anapendekeza kuchelewesha kuanza kwa kesi ya mashtaka dhidi ya Rais wa zamani Marekani, Donald Trump kwa wiki moja au zaidi ili kumpa muda Trump wa kutathmini kesi hiyo.

Wabunge wa Democratic ambao walipiga kura ya kumfungulia mashtaka Trump wiki iliyopita kwa kuchochea vurugu kwenye jengo la Bunge hapo Januari 6 wanaashiria kwamba wanataka kesi isikilizwe haraka wakati Rais Joe Biden anaanza muhula wake wakisema kusomewa mashtaka kamili kwa Trump ni muhimu kabla ya nchi na Congress kusonga mbele.

Lakini McConnell aliwaambia maseneta wenzake wa GOP kwenye simu kwamba ucheleweshaji mfupi utampa muda Trump wa kutathmini kesi hiyo na kusimama na timu yake ya wanasheria inayohakikisha mchakato unaofaa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG