Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 10:31

Ufaransa yachukua hatua ya kwanza kujumuisha haki ya kutoa mimba katika katiba


Watu wakusanyika nje ya jengo la baraza kuu la Bunge kuonyesha kuunga mkono hatua ya kupitisha haki ya kutoa mimba, nchini Ufaransa.

Wabunge wa baraza kuu la Bunge nchini  Ufaransa Alhamisi walipitisha mswaada unaojumuisha haki ya kutoa mimba katika katiba ya nchi, ikiwa ni hatua ya kwanza ndefu na mapambano ya kisheria yasiyokuwa na uhakika ambayo yamechochewa na kuzuiliwa kwa  haki ya utoaji mimba nchini Marekani.

Kura iliyopigwa ilikuwa 337-32 katika Bunge la Taifa lenye wajumbe 557.

Ili kuongezwa katika katiba, hatua yoyote lazima kwana iidhinishwe na wabunge wengi katika Bunge la Taifa na baraza la Seneti, halafu kuidhinishwa katika kura ya maoni kitaifa.

Waandishi wa pendekezo hilo, kutoka muungano wa mrengo wa kushoto, walitoa hoja kuwa hatua hiyo inalenga l “kulinda na kutoa dhamana kwa haki ya msingi ya mtu kuwa na hiari ya kutoa mimba.”

Utoaji mimba nchini Ufaransa ulikuwa umefanywa ni uhalifu chini ya sheria kuu ya mwaka 1975, lakini hakuna kilichoandikwa katika katiba ambacho kinaweza kutoa dhamana kwa haki ya utoaji mimba.

Mathilde Panot, mkuu wa kikundi cha mrengo wa kushoto cha France Unbowed katika Bunge la Taifa na mmoja waliosaini pendekezo hilo, alisema kuwa “lengo letu liko wazi: hatutaki kuacha fursa yoyote kwa watu ambao wanapinga haki ya mtu kutoa mimba.”

Waziri wa Sheria wa Ufaransa Eric Dupond-Moretti alisema kuwa serikali ya mrengo wa kati inaunga mkono juhudi hii.

Alikuwa anaongelea juu ya uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Marekani mwezi Juni, ambao ilifuta haki ya kikatiba ya serikali kuu juu ya utoaji mimba na kuacha uamuzi huo ufanyike katika ngazi ya majimbo.

“Haki ya kutoa mimba tulidhani kuwa ilikuwa tayari imefikiwa miaka 50 iliyopita [nchini Marekani] lakini kiuhakika haijafikiwa kabisa,” alisema.

Ukusanyaji maoni wa hivi karibuni ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 80 raia wa Ufaransa wanaunga mkono haki ya kutoa mimba. Matokeo ya utafiti huu yanalingana na yale yaliyofanyika siku za nyuma. Kura hiyo ya maoni ilionyesha pia idadi ya kutosha ya watu wengi wanapendelea haki ya kutoa mimba iwekwe katika kat

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG