Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 09:48

Ufaransa haijafuta uwezekano wa kuondoa vikosi vyake Burkina Faso


Rais wa Ufaransa, Emanuel Macron
Rais wa Ufaransa, Emanuel Macron

Lakini chuki imekuwa ikiongezeka katika koloni hilo la zamani la Ufaransa baada ya miaka mingi ya juhudi za kupambana na wanajihadi ambazo zimeshindwa kuzuia mashambulizi ya uasi yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimisha mamilioni wengine kuyakimbia makaazi yao

Ufaransa haijafuta uwezekano wa kuondoa vikosi vyake maalum nchini Burkina Faso ambako maandamano dhidi ya uwepo wa jeshi la Ufaransa yamekuwa yakiongezeka Waziri wa Ulinzi Sebastien Lecornu alisema katika mahojiano yaliyochapishwa Jumapili.

"Tathmini ya mkakati wetu kwa jumla barani Afrika inatutaka kuhoji masuala yote ya uwepo wetu, ikiwa ni pamoja na vikosi vyetu maalum," Lecornu aliliambia gazeti la Journal du Dimanche.

Kikosi cha Sabre kilichopo karibu na mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou "kimekuwa na jukumu muhimu katika vita dhidi ya ugaidi huko Sahel", Lecornu ameongeza.

Lakini chuki imekuwa ikiongezeka katika koloni hilo la zamani la Ufaransa baada ya miaka mingi ya juhudi za kupambana na wanajihadi ambazo zimeshindwa kuzuia mashambulizi ya uasi yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimisha mamilioni wengine kuyakimbia makaazi yao.

Siku ya Ijumaa polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya umati wa mamia kadhaa ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kuelekea ubalozi wa Ufaransa mjini Ouagadougou.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mwezi huu alimaliza rasmi operesheni ya Barkhane ambayo imekuwa ikizisaidia nchi za Sahel kupambana na uasi wa Kiislamu, akitangaza tathmini ya miezi sita ya mkakati wa kijeshi wa Ufaransa kwa eneo hilo.

Macron aliwaondoa wanajeshi wa Ufaransa kutoka nchi jirani ya Mali mapema mwaka huu huku uhusiano ukidorora na watawala wa kijeshi walioiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa katika mapinduzi ya mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG