Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 20:37

Mfahamu Mike Pence mgombea mwenza wa mrepublican Donald Trump


 Mike Pence gavana wa Indiana, mgombea menza wa mrepublican Donald Trump
Mike Pence gavana wa Indiana, mgombea menza wa mrepublican Donald Trump

Katika miezi ya karibuni tangu mgombea urais wa Republican Donald Trump kumtaja mgombea mwenza wake, gavana wa Indiana Mike Pence, kwa kiasi imethibitika kwamba ni mfuasi mkubwa wa tajiri huyo.

Wakati mara kwa mara akitakiwa kuunga mkono matamshi ya Trump au familia yake, mara nyingine ameonekana haogopi kusema kilicho katika mawazo yake.

Michael Richard “Mike” Pence alizaliwa Juni 7 mwaka 1959, huko Columbus Indiana. Ni mmoja wa watoto sita wa Nancy na Edward Pence, mwanajeshi wa zamani katika jeshi la Marekani ambaye alikuwa na vituo kadhaa vya mafuta. Mike Pence alishawishika kuingia katika siasa kutokana na familia kuelemea katika ukatoliki wa Irishi.

Alikua akimpenda rais wa zamani John F. Kennedy na kufanya kazi za kujitolea kwenye chama cha Democratic alipokuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari.

Pence alihitimu kutoka chuo cha Hannover akiwa na shahada ya historia na kuhamia Indianapolisi mwaka 1983 na kuhudhuria chuo kikuu kikuu cha Indiana katika shule ya sheria ya Mckinney na kuhitimu 1986 na kujiajiri.

Baada ya kushindwa mara mbili alipowania ubunge mwaka 1988 na 1990, alikuwa mtangazaji mconservative kwenye radio na televisheni kuanzia mwaka 1994 mpaka 1999. Na kujiita mwenyewe kama ‘Rush Limbaugh lakini mwenye msimamo usio mkali,’ Pence hajawahi kujihisi vibaya kwa kuunga mkono ajenda ya kiconservative, lakini alipongezwa kwa utulivu wake na kuwa tayari kusikiliza mawazo tofauti na yake.

Pence aliifufua tena azma yake ya kuingia katika ulingo wa siasa kwa kuwania tena ubunge mwaka 2000, mara hii alishinda. Msimamo wake wa kisiasa umebadilika sana tangu wakati huo. Anapenda kujielezea mwenyewe kama ‘mkristo, mconservative na mrepublican.’

Pia ameeleza bayana kwamba si mtu ambaye atafuata kila kitu kinachoamuliwa na chama chake.

Alipinga sera ya elimu ya rais George W. Bush mwaka 2001 ya "No child Left Behind", pamoja na upanuzi wa huduma ya afya kuhusu madawa mwaka uliofuata. Kwa kufanya hivyo, alibainisha tabia yake kuwa ni mtu mwenye msimamo thabiti na hivyo kushinda tena uchaguzi mara tano kiurahisi.

Pence aliwania uganvana na kushinda kuongoza jimbo la Indiana mwaka 2012. Alizungumziwa sana mwaka jana alipotia saini mswaada wa uhuru wa dini kuwa sheria.

Pence alisema ungeongeza ulinzi wa kisheria kwa wamiliki wa biashara wa Indiana ambao hawakutaka kushiriki katika ndoa za watu wa jinsia moja, wakielezea imani za kidini, wapinzani wa hilo walidai kwamba alikuwa analeta ubaguzi.

Vile vile, alishutumiwa mapema mwaka huu kwa kutia saini mswaada ambao unapiga marufuku utoaji mimba hata kama uja uzito una matatizo.

Pence amemuoa Karen, tangu mwaka 1985. Mwalimu wa zamani wa shule ya msingi. Karen pia amehusika katika taasisi zisizo za kiserikali kuhusu vijana. Wawili hao wana watoto watatu, Michael, Charlotte na Audrey.

XS
SM
MD
LG