Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 02:14

Mali yapiga marufuku Mashirika yasiyo ya serikali yanayofadhiliwa na Ufaransa


Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Mali.
Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Mali.

Serikali ya kijeshi  ya Mali Jumatatu ilipiga marufuku shughuli za mashirika yasiyo ya serikali yanayofadhiliwa au kuungwa mkono na Ufaransa, ikiwa ni pamoja na mashirika ya kibinadamu, huku kukiwa na mzozo unaozidi kuwa mbaya kati ya Paris na Bamako.

Waziri Mkuu wa muda wa taifa hilo la Afrika Magharibi Kanali Abdoulaye Maiga alihalalisha hatua hiyo katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, na kuitaja kuwa ni jibu kwa Ufaransa kusitisha misaada ya maendeleo kwa Mali hivi karibuni.

Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilisema wiki iliyopita ilifanya uamuzi huo, ambao ulikuja miezi mitatu baada ya kukamilisha mchakato wa kuviondoa vikosi vyake, vya kupambana na wapiganaji wa Kiislamu, kutoka nchi hiyo, juu ya madai ya Bamako ya kutumia wanamgambo wa kundi la Wagner la Russia.

Wiki iliyopita, chanzo cha wizara ya mambo ya nje kilisema Ufaransa itadumisha misaada yake ya kibinadamu pamoja na kufadhili "mashirika ya kiraia" nchini Mali.

XS
SM
MD
LG