Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 03:33

Ujerumani yadaiwa kujiondoa kulinda amani Mali


Ujerumani itasimamisha ushiriki wake wa kulinda amani chini ya tume ya Umoja wa Mataifa ya Mali.

Hilo litafanyika itakapofika mwishoni mwa mwaka ujao chanzo kimoja cha serekali kimelieleza shirika la habari la AFP baada ya kufanya oparesheni zake.

Shirika la habari la AFP linaripoti kwamba chanzo hicho kimesema itakapofika mwishoni mwa mwaka 2023, wanajeshi wa Ujerumani watamaliza ushiriki wao katika kulinda amani chini ya tume ya Umoja wa Mataifa MINUSMA.

Uingereza na Ivory Coast mapema wiki hii walitangaza kujiondoa katika ulinzi wa amani Mali.

Kwa mujibu wa vyanzo vya Ujerumani, maafisa kutoka ofisi ya kansela, wizara ya ulinzi na mambo ya nje walifikia makubaliano ya kuondoa vikosi.

Uamuzi wa mwisho wa kama kuendelea kuwepo Mali utafanyika Jumanne katika mkutano utakao hudhuriwa na kansela Olaf Scholz, chanzo hicho kimesema.

XS
SM
MD
LG