Kulingana na mkataba mpya, Uingereza inatakiwa kuilipa Ufaransa dola za Marekani milioni 75 kuimarisha ulinzi ambao utawazuia wahamiaji na wanaoomba hifadhi kutumia boti ndogondogo kuvuka kutoka Ufaransa kupitia mkondo hatari wa maji.
Makubaliano hayo yanaongeza doria kwa asilimia 40 na kuongeza matumizi ya droni na teknolojia nyingine kuwazuia watu hao kuvuka.
Mkataba huo pia unaeleza kuwa nchi hizo mbili zitashirikiana taarifa kuhusu magendo na kero nyingine zilizopatikana kutoka kwa wahamiaji waliokamatwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman walisaini mkataba huo Jumatatu mjini Paris.
Baadhi ya taarifa hizi katika ripoti hii zinatokana na shirika la habari la AP