Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:48

Maandamano yanafanyika Italy kutetea wakimbizi kutoka Afrika


Wahamiaji waliokamatwa katika bahari ya Mediterrania wakiwa safarini kuelekea Ulaya, wakirudishwa Libya, Mei 23, 2022
Wahamiaji waliokamatwa katika bahari ya Mediterrania wakiwa safarini kuelekea Ulaya, wakirudishwa Libya, Mei 23, 2022

Makundi ya kuetea haki za binadamu yamefanya maandamano mjini Rome, Italy, kupinga kurejesha tena ushirikiano kati ya Italy na Libya, wa kuwazuia wahamiaji na wakimbizi wanaofika pwani ya Ulaya.

Waandamanaji wanadai kwamba haki za binadamu zinakiukwa sana nchini Libya ambako wahamiaji na wakimbizi wanajaribu kuvuka bahari ya Mediterania.

Makubaliano kuhusu ushirikiano, uhamiaji haramu, biashara ya binadamu, biashara ya magendo ya mafuta na kuimarisha usalama mipakani, yamesainiwa na waziri mkuu wa Italy Gentiloni, na mkuu wa serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa Fayez al-Serraj.

Kulingana na makubaliano hayo, Italy ilikuwa ikiipatia Libya msaada wa meli za kupiga doria baharini, pamoja na kutoa mafunzo kwa maafisa wa ulinzi wa bahari ili kukabiliana na uhamiaji haram una usafirishaji wa watu kinyume cha sheria.

Mkataba huo pia unatoa fursa ya kuundwa kwa vituo vya misaada kaskazini mwa Afrika, hasa nchini Libya, ili kuwapa makazi wahamiaji watakaokamatwa baharini wakiwa safarini kuelekea Ulaya.

Lakini mashirika yasiyo ya kiserikali yamesema kwamba ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huwa unafanyika katika vituo hivyo.

"Tupo hapa kwa sababu kuna watu wengi, wanaharakati wengi ambao hawawezi kuendelea kuvumilia haya kwamba serikali ya Italy inaendelea kufadhili wauaji walioko nchini Libya. Pia kuwaweka watu wengi sana katika kambi. Tunawajibika kwa vifo vyao wakiwa baharini nchini Libya," amesema Enrico Calami, mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi

XS
SM
MD
LG