Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 21:45

Maafisa wa Uturuki wajibu tuhuma za Ugiriki

Raia wa Afghanistan aliyefunikwa na blanketi, anazungumza na wahamiaji wengine katika shule ya zamani inayotumiwa kama makazi ya muda kwenye kisiwa cha Kythira, kusini mwa Ugiriki, Ijumaa, Oktoba 7, 2022.

Maafisa wa Uturuki wamejibu tuhuma za Ugiriki kuwa Uturuki iliwalazimisha wahamiaji 92 kuingia Ugiriki.

Uturuki iliziita "habari za uwongo" na ikashutumu Ugiriki kwa unyanyasaji huo. Mkurugenzi wa mawasiliano wa rais wa Uturuki alisema Jumapili kwamba waziri wa uhamiaji wa Ugiriki "anasambaza habari za uwongo" baada ya waziri huyo kutuma picha Jumamosi ya wahamiaji hao wakiwa uchi na kuilaumu Uturuki.

Afisa wa rais wa Uturuki alituma ujumbe kwenye Twitter kwamba hii ilikuwa "kuishuku nchi yetu" huku akitoa wito kwa Athens kuachana na "vitendo vibaya kwa wakimbizi."

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili jirani umekuwa wa wasiwasi kutokana na masuala mbalimbali yakiwemo ya uhamiaji.

XS
SM
MD
LG