Nasa pia imewashutumu polisi ikidai kuwa wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na waandamanaji ambao ni wakazi wa maeneo ambayo ni ngome ya kambi ya upinzani.
"Serikali hii haijafurahi kwamba watu wameikataa, inatumia nguvu kuwakabili wapinzani wake," amesema Musalia Mudavadi.
Vyanzo vya habari Kenya vimesema kuwa Mudavadi ameitaka IEBC kufuta uchaguzi huo.
Uchaguzi huo wa urais ulikuwa umepangwa kufanyika Octoba 28. Kutokana na hali za usalama kaunti nne za magharibi mwa Kenya ambazo ziko katika ngome ya upinzani hazikukamilisha zoezi hilo Octoba 26 uchaguzi wa urais ulipofanyika.Kwa mujibu wa IEBC Kaunti hizo nne ni Kisumu, Migori, Siaya na Homa Bay.
Vyombo vya usalama vimesema maeneo hayo yalikabiliwa na vurugu na mapambano kati ya waandamanaji na polisi wakati ikiwa ni harakati za upinzani kupinga kufanyika marudio ya uchaguzi huo.
Vyanzo vya habari vimesema kuwa Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema IEBC imechukua hatua hiyo ili kulinda maisha ya wafanyakazi wake.