Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 14:44

UAE yafuta sheria ya kuisusia Israeli


Ukumbi wa Tel Aviv City Hall ukipeperusha bendera ya UAE wakati Israel na UAE walipotangaza kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia huko Tel Aviv, Israeli, Agosti. 13, 2020.
Ukumbi wa Tel Aviv City Hall ukipeperusha bendera ya UAE wakati Israel na UAE walipotangaza kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia huko Tel Aviv, Israeli, Agosti. 13, 2020.

Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ametoa amri ya kiutendaji inayofuta sheria ya kuisusia Israeli na kuruhusu mikataba ya biashara na fedha kati ya nchi hizo mbili, shirika la habari la serikali WAM limeripoti Jumamosi.

Amri hiyo ya kiutendaji kutoka kwa Rais wa UAE Khalifa bin Zayed Al Nahyan inalenga katika “kuunga mkono ushirikiano wa pande mbili kwa ajili ya kufikia (kuwepo) kwa mahusiano kati ya nchi hizo”, shirika la habari la Reuters limeripoti.

Tangazo hilo linakuja wakati shirika la ndege la Israel, El Al likipanga kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya uwanja wa ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv na mji mkuu wa UAE, Abu Dhabi.

Ndege hiyo itakuwa na ujumbe wa ngazi ya juu wa Israeli na wasaidizi wa ngazi ya juu wa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alisimamia makubaliano ya kurudisha mahusiano kati ya Israeli na UAE Agosti 13, 2020.

Mshauri wa ngazi ya juu wa Trump Jared Kushner atakuwa kati ya maafisa wa Marekani katika ndege hiyo ya El Al itakayoanza safari yake Agosti 31 saa nne za asubuhi (0700GMT) afisa mmoja wa Marekani ameeleza.

Makubaliano kati ya Isreal-UAE yanasubiri mazungumzo kuhusu maelezo ya namna ya kufungua balozi baina yao, biashara na muungano wa safari kabla ya kusainiwa rasmi.

Hakuna mahusiano ya safari za ndege kati ya Israeli na UAE, na haikuwekwa wazi iwapo El Al itaweza kurusha ndege yake katika anga ya Saudi Arabia, ambayo haina mahusiano rasmi na Israeli, ili kupunguza muda wa safari hiyo.

Mwezi May, ndege ya shirika la ndege la Etihad lilifanya safari yake kutoka UAE kwenda Tel Aviv kupeleka mahitaji kwa Wapalestina kwa ajili ya kutumika katika janga la virusi vya corona, ikiwa ni safari ya kwanza inayojulikana iliyofanywa na ndege ya UAE kwenda Israeli.

XS
SM
MD
LG