Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 22:47

Tetemeko lasababisha vifo vya watu 8 Indonesia


Mtu akijaribu kuvitoa vitu vilivyo kuwa ndani ya nyumba iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi huko Lumajang, mashariki ya jimbo la Java, Indonesia, 11 April 2021. Picha na Antara Foto/Zabur Karuru/via REUTERS (Foto: Antara/Zabur Karuru via REUTERS)

Tetemeko kubwa la ardhi limepiga kisiwa cha Java nchini Indonesia na kuua watu wanane.

Waliokufa ni pamoja na mwanamke ambaye pikipiki yake iligongwa na mawe yaliyokuwa yanaporomoka, na kuharibu zaidi ya majengo 1,300, maafisa wamesema hivi leo Jumapili.

Tetemeko hilo halikusababisha tsunami. Idara ya Marekani ya jiolojia imesema kiwango cha tetemeko chenye ukubwa wa 6. katika kipimo cha rikta kimepiga kisiwa hicho cha pwani ya kusini saa nane mchana siku ya Jumamosi.

Kilikuwa katika eneo la kati ya kilometa 45 kusini mwa mji wa Sumberpucuung katika wilaya ya Malanga katika jimbo la Java Mashariki.

Rahmat Triyono, mkuu wa kituo cha tetemeko la ardhi na tsunami nchini Indonesia amesema mitetemo ya chini ya bahari haikusababisha tsunami.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG