Shirika la kupambana na majanga nchini humo, limesema hayo Jumapili na kueleza kuwa matope yaliporomoka kutoka milima inayozunguka vijiji vilivyoathiriwa, muda mfupi baada ya saa sita usiku na kuharibu takriban nyumba 50 katika kijiji cha Lame-nele kwenye Kisiwa cha Flores, katika mkoa wa mashariki wa Nusa Te-ngara.
Waokoaji walipata miili 20 na majeruhi tisa, alisema Raditya Jati, msemaji wa shirika la Kitaifa la kupambana na majanga. Miili mingine mitatu ilipatikana ya wanakijiji ambao walisombwa na mafuriko katika kijiji cha Oyang Bayang.
Mvua hizo za usiku zilisababisha mito kufurika, na maporomoka makubwa ya ardhi.
Mamia ya watu walikimbia nyumba zilizokuwa zimezama, ambazo zingine zilisombwa na mafuriko, Jati alisema.
Mamia ya watu walihusika katika juhudi za uokoaji, lakini usambazaji wa misaada ulikwamishwa na kukatwa kwa umeme, barabara zilizofungwa na umbali wa eneo ambalo, limezungukwa na maji machafu na mawimbi makubwa, kwa mujibu wa maafisa wa serikali.
Mafuriko makubwa pia yameripotiwa katika mji wa Bima, ulioko katika jimbo jirani la Magharibi mwa Nusa Tenggara, na kulazimisha karibu watu 10,000 kukimbia, Jati alisema.