Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:43

Sikukuu ya Matawi : Wawili wajilipua kwa mabomu nje ya Kanisa Indonesia


Polisi wakilinda doria nje ya Kanisa Katoliki, huku njia zikiwa zimefungwa baada mlipuko wa mabomu,kwenye mji mkuu Makassar, katika jimbo la Sulawesi, Indonesia, Machi 28, 2021. Picha na Antara Foto. Antara Foto/Arnas Padda/ via REUTERS.
Polisi wakilinda doria nje ya Kanisa Katoliki, huku njia zikiwa zimefungwa baada mlipuko wa mabomu,kwenye mji mkuu Makassar, katika jimbo la Sulawesi, Indonesia, Machi 28, 2021. Picha na Antara Foto. Antara Foto/Arnas Padda/ via REUTERS.

Walipuaji mabomu wawali wa kujitoa mhanga wametegua milipuko Jumapili kwenye mlango mkuu wa kuingia kwenye Kanisa Katoliki katika maadhimisho ya sikukuu ya Matawi Indonesia. 

Tukio hilo limetokea katika kisiwa cha Sulawesi ambapo watu takriban 20 wamejeruhiwa, polisi imesema.

Video iliyochukuliwa na shirika la Habari la AP imeonyesha miili ya watu ikiwa imekatika karibu na pikipiki iliyounguwa kwenye mlango wa kuingia kwenye kanisa hilo maarufu kama Jesus Cathedral kwenye mji mkuu Makassar katika jimbo la Sulawesi.

Kasisi Wilhelmus Tulak wa Kanisa hilo alikuwa amemaliza ibada ya sikukuu ya matawi wakati mlio mkubwa uliposikika na kuzusha taharuki kwa waliokuwepo hapo.

Amesema mlipuko ulitokea majira ya saa 10:30 asubuhi kwa saa za Indonesia wakati watu wakitoka kanisani na kundi jingine lilikuwa linaingia kwa ibada ya pili.

Amesema walinzi wa kanisa walikuwa na wasiwasi kuhusu wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki waliotaka kuingia kanisani na walipozuiwa walijilipua.

Hata hivyo polisi imesema washambuliaji walikufa papo hapo na ushahidi uliokusanywa unaonyesha mmoja kati ya hao alikuwa mwanamke. Miongoni mwa waliojeruhiwa ni pamoja na walinzi wanne na waumini wa kanisa hilo.

XS
SM
MD
LG