Vifo hivi vimetokea katika visiwa vya kusini mashariki ya nchi hiyo na Timor mashariki, huku watu wengi hawajulikani walipo.
Idara ya dharura BNPB inasema kwamba kuna karibu watu wengine 70 wamefariki katika visiwa vya Indonesia magharibi ya majimbo ya Nusa Tenggara mashariki huku 70 wengine hawajulikani walipo.
Hii ni baada ya kimbunga kusababisha mafuriko ya ghafla, maporomoko ya ardhi na upepo mkali kukiwa na mvua nyingi mwishioni mwa wiki.
Nchini Timor Mashariki karibu watu 27 wameuliwa kutokana na maporomoko ya ardhi na maafisa wanasema watu 7,000 wamepoteza makazi yay.