Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 14:52

Jordan yaonya usalama wa mfalme ni 'mstari mwekundu' hauvukwi


Prince Hamza

Spika wa Baraza la Seneti la Jordan, Faisal al-Fayez amesema Jumapili Usalama wa Jordan na Mfalme Abdullah wa pili ni “mstari mwekundu” mtu hauvuki, alipokuwa ana hutubia mkutano maalum wa bunge kuadhimisha miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa utawala wa kifalme. 

Matamshi yake yametolewa siku moja tu baada ya maafisa kadhaa waandamizi kukamatwa pamoja na kaka wa kambo wa Mfalme Abdulla wa pili, ambaye amewekwa kizuizini nyumbani.

Picha za video zilizochapishwa kwenye mitandao zinaonyesha kuwepo na ulinzi mkali wa polisi katika mtaa wa Daouq karibu na kasri ya Mfalme pamoja na maeneo yanayouzungukla mji mkuu wa Amman, wakati mwanamfalme mrithi Hamzah bin Hussein amefungiwa nyumbani kwake.

Hamzah bin al-Hussein amesema katika picha ya video iliyorikodiwa Jumamosi kuwa yuko kizuizini nyumbani na ametakiwa kutowasiliana na mtu yoyote.

Ametoa tamko hilo lililorikodiwa baada ya jeshi la nchi hiyo kumtaka asitishe harakat zote zilizotumika kuyumbisha “utulivu na usalama” wa nchi hiyo.

Hamzah ameeleza katika video hiyo, iliyowasilishwa na mawakili wake kwa idhaa ya Uingereza, ya BBC kuwa alikuwa hahusiani na njama zozote za kigeni na kulaani kile anachosema ni utawala wa ulaji rushwa nchini humo.

“Ni hatua ya kusikitisha na kuhuzunisha,” ameongeza kusema.

Katika taarifa, iliyochapishwa katika shirika la habari la serikali, jeshi linamesema linafanya uchunguzi wa kina kuhusu usalama ambapo waziri wa zamani, mwanafamilia wa familia ya kifalme na wengine waliokuwa hawajatajwa wamewekwa kizuizini.

Gazeti la Washington Post limesema maafisa wa serikali nchini Jordan wanamshikilia Hamzah na wamewakamata takriban watu wengine 20 kufuatia kile maafisa walichokiita “tishio kwa utulivu wa nchi hiyo.”

Afisa wa zamani wa Marekani ambaye anafahamu matukio hayo nchini Jordan amesema tishio hilo halikuhusisha mapinduzi. Lakini, amesema, wale wote waliohusika walikuwa wanapanga kushinikiza kuwepo maandamano ambayo yangeonekana ni “maandamano ya wananchi yanayou mkono na wengi mitaani” yakiungwa mkono na makabila.

Mwana wa mfalme Hamzah haonekani kuwa ni tishio kubwa kwa utawala wa kifalme wa Jordan, na tayari kwa miaka mingi ametengwa.

Lakini wakuu wa serikali wameanza hiyo na wasiwasi na juhudi zake za kujenga mahusiano na viongozi wenye hasira katika makabila yalio na nguvu.

Makabila hayo yanashikilia nafasi muhimu katika vikosi vya usalama na jeshi na wasaidizi wakuu wa utawala wa kifalme wa Hashemite.

Shirika la habari la serikali limewataja wawili kati ya waliowekwa kizuizini : Bassem Awadallah, aliyesoma Marekani na aliyeaminiwa kwa muda mrefu na mfalme na baadae kupewa nafasi ya waziri wa fedha na ni mshauri wa mwana wa mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman; na Sharif Hassan bin Zaid, mjumbe wa familia ya kifalme. Lakini hapakuwa na maelezo zaidi.

Kasri ya mfalme wa Saudi Arabia imeeleza “kumuunga mkono kikamilifu” Mfalme Abdallah na maamuzi yake yote ya kuimarisha usalama na utulivu. Misri, Lebanon na Bahrain zimemuunga mkono mfalme wa Jordan.

“Tunafuatilia kwa karibu kufuatia ripoti hizi na tunawasiliana na maafisa wa Jordan,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price amesema katika ujumbe wa barua pepe Jumamosi.

“Mfalme Abdullah ni mshirika mkuu wa Marekani, na tunamuunga mkono kikamilifu.”

Mfalme Abdullah wa Jordan
Mfalme Abdullah wa Jordan

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG