Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:17

Waziri Mkuu wa Iraq akutana na wafanyabiashara wa Saudi Arabia


Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhemi
Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhemi

Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhemi anakutana na wafanyabiashara wa Saudi Arabia wakati wa ziara yake iliyosubiriwa kwa muda mrefu katika ufalme huo.

Ziara yake inalengo la kuunda tena uhusiano wa karibu wa kiuchumi na usalama.

Safari ya Kadhemi inafanyika baada ya nchi hizo kufungua tena kituo cha kuvuka mpaka cha Arar Novemba kwa mara ya kwanza tangu Riyadh ilipovunja uhusiano wa kidiplomasia na Baghdad mwaka 1990, kufuatia uvamizi wa dikteta wa zamani wa Iraq Saddam Hussein dhidi ya Kuwait.

Japo inafahamika kwamba ana uhusiano wa karibu wa kibinafsi na mwana mfalme mrithi Mohammed, lakini al-Kadhemi anajikuta katika hali ngumu mara nyingi akitumbukia katika mivutano inayoendelea kati ya Tehran na mahasimu wake Riyadh na Washington.

Mbali na majadiliano juu ya usalama wa mipaka, Waziri Mkuu wa Iraq alisema yeye na ujumbe wake wa mawaziri waandamiziwalitaka kuongeza zaidi ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi na ufalme wakati wa ziara ya siku moja huko Riyadh.

XS
SM
MD
LG