Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 01, 2023 Local time: 16:29

Papa Francis azuru makanisa yaliyo haribiwa na Islamic State Iraki


Papa Francis, akiwa katika eneo la makanisa yaliyo haribiwa na kundi la Islamic State na kuwaombea wahanga wa vita vya kanisa la Hosh al-Bieaa huko mjini Mosul, Iraki, Jumapili, Machi 7, 2021.

Papa Francis amewasili kaskazini mwa Iraq Jumapili ambako alisali kwenye mabaki ya makanisa yaliyo haribiwa na Islamic State na pia alifanya misa ya wazi.

Kituo chake cha kwanza kilikuwa mjini Mosul, ambako iliwahi kuwa ngome ya Islamic State.

Alisali kuwaombea waathirika wa vita nchini Iraq kwenye eneo la city square, miongoni mwa mabaki ya makanisa kadhaa ambayo yalivunjwa kabisa na wanamgambo.

Baada ya Mosul, baadaye Papa Francis alielekea Qaraqosh, mji wa kale wa Kikristo ambao uliovamiwa na majeshi ya Islamic State, ambako alikutana na wanachama wa jamii za kieneo katika Kanisa la Immaculate Conception.

Papa alifanya misa ya wazi kwenye uwanja wa Franso Hariri mjini Erbil kabla ya kurejea mjini Baghdad.

Kwasababu ya masharti ya Covid 19, mahudhurio ya ibada hiyo yalikuwa ni kwa watu elfu kumi tu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG