Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 20:17

Papa ataka sheria kuundwa kuwalinda mashoga 


Picha ya zamani ya Papa Francis mjini Vatican, Oct. 21, 2020. (Reuters)
Picha ya zamani ya Papa Francis mjini Vatican, Oct. 21, 2020. (Reuters)

Watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja wanastahili kupata haki ya kuwa na  familia. Hakuna anayestahili kutengwa au kufanywa kujihisi kutengwa kwa sababu ya hilo, asema Baba Mtakatifu.

Kiongozi wa kanisa Papa Francis amesema kwamba watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja wanastahili kulindwa na sheria za mahusiano.

Matamshi ya Papa Francis yamenukuliwa kutoka kwa video mpya ambayo imetolewa Jumatano.

Amesema kwamba “watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja wanastahili kupata haki ya kuwa na familia. Hakuna anayestahili kutengwa au kufanywa kujihisi kutengwa kwa sababu ya hilo. Tunachostahili kufanya ni kuunda sheria ya kulinda uhusiano wao. Kwa njia hiyo, watalindwa kisheria. Nilisimama na hilo.”

Kwa kusema kwamba “alisimama na hilo,” Papa Francis aliashiria kufafanua msimamo wake wakati alipokuwa askofu mkuu wa Buenos Aires, ambapo alipinga mchakato wa kuunda sheria ya kuidhinisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja lakini akaunga mkono uundwaji wa sheria kuwalinda watu walio katika uhusiano huo.

Mwelekezi wa filamu ambayo Papa Francis amenukuliwa akisema hayo, Evgeny Afineevsky amesema kwamba “nadhani anatufanya tuelewe kwamba sisi ndio tulio na msimamo mbaya dhidi ya watu wa jinsia moja walio katika uhusiano wa kimapenzi, na kwamba tunajiundia mambo mabaya wenyewe. Lakini wakati huo huo, anaturuhusu kuelewa kwamba hata tunapofanya makosa tunaweza kukiri makosa hayo na kubadilika.”

Filamu hiyo kwa jina "Francesco," imeonyeshwa katika tamasha la filamu mjini Rome, Jumatano.

Inamuweka papa Francis katikati ya mjadala nafasi kuhusu matatizo kadhaa yanayoisumbua sana dunia kwa sasa.

Inaangazia maswala kama pengo linaloendelea kupanuka kati ya masikni na tajiri, ubaguzi wa rangi, mabadiliko ya hali ya hewa, dhuluma za kingono, uhamiaji, ulanguzi wa watu na uhusiano kati ya wakiristo, waislamu na wayahudi.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG