Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:34

Tanzania yatangaza mgao wa umeme baada ya viwango vya maji kushuka


Mgao wa umeme utaendelea kwa muda Tanzania.
Mgao wa umeme utaendelea kwa muda Tanzania.

Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, linasema baadhi ya maeneo ya sehemu za nchi zinatarajiwa kutumia karibu nusu ya siku bila ya umeme. Mji mkuu wa kibiashara umekuwa katika mgao wa maji kwa wiki kadhaa hivi sasa.

Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, linasema baadhi ya maeneo ya sehemu za nchi zinatarajiwa kutumia karibu nusu ya siku bila ya umeme. Mji mkuu wa kibiashara umekuwa katika mgao wa maji kwa wiki kadhaa hivi sasa.

Mkazi wa Dar es Salaam Ramadhani Ibrahim ambaye anajikimu kimaisha kwa kuwa na kituo cha kujaza umeme kwenye matairi ya magari na baiskeli, lakini hivi sasa biashara yake imeshuka kutokana na changamoto za umeme.

Anasema shughuli hii ya kujaza upepo kwenye matairi inatusaidia sana kujipatia fedha kidogo ili kujikimu kimaisha. Lakini mashine tunayotumia inahitaji umeme na umeme mara upo mara umekatika na hatufahamu ni muda utarejea. Kwahiyo Ibrahim anasema umeme ukiwa haupo, anaacha kufanya kazi.

Mamlaka zinasema usambazaji umeme kupitia gridi ya taifa umeshuka kwasababu ya vipindi virefu vya ukame na matengenezo yanayoendelea katika baadhi ya vinu vya kuzalisha umeme. Baadhi ya maeneo yanakabiliwa mpaka muda wa saa tisa kwa siku bila ya umeme.

Kampuni ya ugavi wa umeme inasema uhaba wa umeme katika nchi kwa siku ni kati ya megawati 300 na 350. Maharage Chande meneja wa Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO anasema, “miongoni kwa juhudi za muda mfupi ambazo tunazitekeleza hivi sasa ni kuelekeza uwezo wetu kwenye viwanda vya gesi. Na pia, kushughulikia na juhudi zinazoendelea za matengenezo kwenye viwanda vyetu ili kupunguzza uhaba wa sasa wa umeme.” Chande aliongezea kwamba kiwanda cha kwanza ambacho tunasisitiza ni kupanua kiwanda cha Ubungo 3, ambako tuna mashine mbili zenye uwezo wa kuzalisha megawati 80 za umeme ambako matengenezo yanaendelea.”

Tanzania inafanya kazi kuongeza uwezo wa uzalishaji umeme wa maji, ikiwa ni pamoja na kuendeleza. Ujenzi wa mradi wa bwawa kubwa la Julius Nyerere katika hifadhi ya Selous, ambapo likikamilika linatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 za. Umeme.

Martin Mwambene ni kaimu mkurugenzi kwa wateja na huduma katika kampuni anasema “mradi huu wa bwawa hili ni miongoni mwa mikakati mikubwa ambayo itakuja kushughulikia changamoto za umeme kwa kiwango kikubwa. Hivi sasa, tumefikia asilimia 77 mpaka kukamilika lakini mradi huu unakwenda sambamba na miradi mingine, ikiwemo uzalishaji umeme kwa nishati ya jua. Kadri muda unavyokwenda, Mwambene anaongezea, watakamilisha hilo na kuifanya hali ya umeme kuwa wa uhakika.

Wanaharakati wa halli ya hewa, kama Venance Majula anasema mengi zaidi yanahitaji kufanya kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa nchini.

“Tunahitaji kuwekeza katika hatua za hali ya hewa ikiwemo nyenzo za hifadhi ya mazingira, kilimo ambacho ni rafiki kwa hali ya hewa lakini pia kuwekeza katika nishati mbadala. Bila ya juhudi muafaka, mabadiliko ya hali ya hewayataleta changamoto zaidi kwa utawala wa maji na nishati na pia kusababisha matukio makubwa sana ya hali ya hewa kama vile mafuriko na ukame kama tunavyoona katika sehemu tofauti za bara hili.,” anasema Majula.

Ukame umelipiga eneo la Afrika Mashariki, huku majirani wa Tanzania upande wa kaskazini Kenya, Somalia na Ethiopia wakikumbana na ukame mbaya sana ambao umechangiwana misimu minne ya mvua zisizo na uhakika.

Mikoa ya Dar es Salaam na Pwanio inatumia asilimia 50 ya mahitaji ya umeme Tanzania. Huku viwanda vingi vipo katika mikoa hiyo, uhaba pia huenda ukaathiri uzalishaji.

((Charles Kombe, VOA News, Dar es Salaam, Tanzania))

XS
SM
MD
LG