Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 20:03

Ndege ya Precision: Samia ameitisha kikao cha mawaziri baada ya wavuvi kuongoza uokoaji


Waokiaji wakiendelea kutafuta manusura katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyokuwa imebeba watu 43 kuanguka katika ziwa Victoria, Bukoba, Tanzania Nov 6, 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameitisha kikao cha dharura cha baraza la mawaziri, kujadili kilichosababisha ajali ya ndege ya Precision huku kukiwepo ripoti za uzembe katika uokoaji.

Watu 19 walifariki kutokana na jail hiyo wiki moja iliyopita, karibu na uwanja wa ndege wa Bukoba, eneo la Kagera.

Msimamizi wa mawasiliano ya rais Zuhura Yunus, ameambia waandishi wa habari katika ikulu ya rais mjini Dar-es-salaam kwamba Kikao hicho kitafanyika Novemba 14 mjini Dodoma.

Rais Samia ameitisha kikao hicho cha baraza la mawaziri huku raia wa Tanzania wakitaka serikali kueleza namna ilivyoshughulikia ajali hiyo kutokana na kile kilichoonekana kama utepetevu wa maafisa husika.

Ndge ya Precision air ilianguka katika ziwa Victoria Jumapili, Nov 6, 2022.

Taarifa za awali zilisema kwamba ilianguka kutokana na hali mbaya ya hewa.

wavuvi waliongoza uokoaji wa watu waliokuwa kwenye ndege hiyo, na kuna ripoti kwamba ilichukua muda mrefu kwa maafisa wenye utaalam kusimamis shughuli ya uokoaji.

Uokoaji wa abiria kwenye ndege hiyo ulifanywa na wavuvi huku watu wa kawaida wakitumia Kamba kuivuta ndege.

Watanzania wanataka serikali kueleza kama ina mikakati yoyote ya kukabiliana na majanga yanapotokea.

Uchunguzi kuhusu kilichosababisha ajali ya ndege hiyo unaendelea na ripoti ya awali inatarajiwa kutolewa mwishoni mwa wiki ijayo (siku 14 tangu ajali ilipotokea).

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG