Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:58

Mahakama ya Arusha yafuta mashtaka ya mauaji ya afisa wa polisi kwa waandamanaji 25 wa Kimasai


Mwanamke Mmasai akitembea katika eneo la hifadhi la Ngorongoro, kaskazini mwa Tanzania. Picha ya AFP
Mwanamke Mmasai akitembea katika eneo la hifadhi la Ngorongoro, kaskazini mwa Tanzania. Picha ya AFP

Mahakama moja ya Tanzania Jumanne imeamuru kuachiliwa kwa zaidi ya waandamanaji 20 wa Kimasai baada ya mwendesha mashtaka kufuta mashtaka ya mauaji ya afisa wa polisi katika maandamano dhidi ya kuwahamisha katika eneo la hifadhi lililotengwa, wakili wao amesema.

Wafugaji hao wa Loliondo katika wilaya ya kaskazini ya Ngorongoro waliishtumu serikali kwa kujaribu kuwalazimisha kuondoka kwenye ardhi ya mababu zao ili kuandaa mashindano ya uwindaji kwa watalii kutoka nje.

Lakini serikali ilitupilia mbali tuhuma hizo, ikidai kuwa inataka kulinda kilomita za mraba 1,500 za eneo hilo kutokana na shughuli za binadamu ili kusaidia wanyamapori kustawi.

Huku hali ya mvutano ikiongezeka, wakati mwingine maandamano yaligeuka kuwa vurugu, ambapo makabiliano yalizuka mwezi Juni huko Loliondo kati ya polisi na waandamanaji wa Kimasai.

Waandamanaji 25 wa Kimasai walishtakiwa kwa mauaji baada ya afisa wa polisi kufariki katika makabiliano hayo.

Mmasai mmoja aliachiliwa wakati huo lakini wengine walibaki gerezani tangu mwezi Juni.

Wakili wao Yonas Masiaya amesema waendesha mashtaka katika mahakama ya Arusha leo Jumanne wamefuta mashtaka yote.

XS
SM
MD
LG