Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 05:20

Tanzania : Mamlaka ya Hali ya Hewa yatahadharisha mafuriko, yashauri maandalizi ya huduma za dharura


Tanzania
Tanzania

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya siku tano, ambapo imeeleza kuna uwezekano wa kunyesha mvua kubwa inayoweza kusababisha athari nyingine yakiwemo mafuriko.

TMA imeshauri Menejimenti ya Maafa na watoa huduma za dharura pamoja na wadau wengine kuchukua hatua za kuweka mipango stahiki kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.

Mvua hiyo inatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe la Jumamosi mvua hizo imeelezwa zinaweza kuleta taharuki katika usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

TMA imesema kuanzia Jumamosi hadi Machi 31, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na Morogoro.

Imeeleza kuwa Aprili Mosi hadi Aprili 2, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG