Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 06:44

WFP yahamasisha mataifa kuisaidia Somalia


Mafuriko nchini Somalia

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linataka kuwepo na msaada mkubwa wa kimataifa kwa maelfu ya wasomali ambao wameathiriwa na mvua kubwa kuwahi kunyesha katika taifa hilo kwa kipindi cha miongo mitatu.

Mvua zilianza kunyesha mwezi uliopita na kusababisha kusambaa kwa mafuriko na uharibifu katika maeneo ya kati, kusini na kaskazini mwa Somalia.

Kwa kipindi cha takriban muongo mmoja uliopita, Somalia imejitahidi kukabiliana na ukame sugu. Mwaka 2011 ukame ulikuwa mbaya sana, na kuua takriban watu 260,000.

Hivi sasa Somalia ina tatizo tofauti, mvua nyingi sana.

Kiasi cha mwezi mmoja uliopita, Rais Mohammed Abdullah Mohammed aliomba msaada wa kimataifa kuwasaidia maelfu ya watu waliokoseshwa makazi na mafuriko makubwa.

Majibu hayakuwa mazuri sana. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani linasema lina wasi wasi hali itakuwa ngumu zaidi kwa vile janga hilo halipo katika vichwa vya habari duniani.

Idara hiyo inaripoti kuwa takriban watu 300,000 kati ya 700,000 walioathiriwa na mafuriko hawana makazi. Msemaji wa WFP, Bettina Luescher anasema idara yake inafanya kile inachoweza kusaidia katika sekta za makazi na usalama ili kujenga ustahmilivu.

‘Lakini, kwa mara nyingine ena hatuna fedha za kutosha. Tunahitaji kiasi cha $ 120 milioni kuwasaidia watu nchini Somalia mpaka mwisho wa mwezi Oktoba. Kama mnavyofahamu, mwaka jana, tulikuwa tunapambana kuepuka njaa nchini Somalia. Tunalazimia kusukuma kuhakikisha kwamba mafanikio yote ambayo tumeweza kuyapata mwaka jana tulipokuwa na uwezo wa kupambana na njaa yanaendelea kuwepo,” amesema Luescher.

Mapema mwaka huu, Umoja wa Mataifa uliomba $1.5 bilioni ili kuwapatia msaada kiasi cha watu milioni tano walioathiriwa na ukame na mzozo. Chini ya $370 milioni au asilimia 24, ndiyo zimepatikana. Anasema WFP inagawa biskuti zenye virutubisho na kutoa pia resheni ya chakula cha miezi miwili katika baadhi ya maeneo.

Anasema sehemu nyingi hazipitiki kwa njia ya barabaa, kwahiyo wafanyakazi wa misaada wanatumia boti kuwafikia watu ambao wamekatiwa njia za usafiri kwasababu ya mafuriko. Anasema WFP, ambayo inaendesha huduma za usafiri wa kwa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa pia imeongeza helikopta ili kuwasafirisha wafanyakazi wa misaada kwenda maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG