Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 22:43

Takukuru - Tanzania yamshikilia waziri wa zamani Lazaro Nyalandu


Lazaro Nyalandu

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania inamshikilia aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kwa tuhuma za vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Tanzania Nyalandu ambaye alihama kutoka Chama cha Mapinduzi kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amekamatwa Jumatatu saa tisa Alasiri mkoani Singida, na hivi sasa anahojiwa na TAKUKURU.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu jioni hii, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida Joshua Msuya amethibitisha kuwa Nyalandu anahojiwa na TAKUKURU kutokana na kufanya vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa.

"Ni kweli tumemkamata Nyalandu kwa ajili ya kufanya naye mahojiano, kuna mikutano ya kisiasa ambayo wanaifanya na kuna viashiria vya vitendo vya rushwa.Hivyo tumemkamata kwa ajili ya kumhoji.Tunaomba ifahamike tunamhoji kwasababu ya kuwepo viashiria vya vitendo vya rushwa na si kwamba tumemkamata akitoa rushwa," amesema Msuya.

Alipoulizwa kama bado wanamshikilia au laa ,Msuya amejibu wao baada ya kumhoji wamemkabidhi kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa mahojiano zaidi.

Joshua amesema sio kweli kwamba Nyalandu amevamiwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha, kwa sababu kabla ya kuchukuliwa kwa ajili ya kuhojiwa alipewa taarifa na hivyo alikuwa anajua kuwa anahitajika TAKUKURU.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG