Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 02:28

Sudan yatishia kutoshiriki mazungumzo ya Doha


Rais wa Sudan Omar al-Bashir, atishia kujitoa kwenye mazungumzo ya amani ya darfur
Rais wa Sudan Omar al-Bashir, atishia kujitoa kwenye mazungumzo ya amani ya darfur

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anasema nchi yake itajitoa kutoka mazungumzo ya amani ya Darfur huko Qatar na kupanga mazungumzo yake binafsi, kama hakuna maafikiano ya haraka ya mkataba na waasi.

Bwana Bashir aliuambia mkusanyiko wa wafuasi wake huko Darfur, Jumatano kwamba ujumbe wa Sudan utaondoka Doha na kufanya mazungumzo huko Darfur kama hakuna mkataba wowote. Pia alitishia majibu ya kijeshi dhidi ya mtu yeyote ambaye atanyanyua silaha huko Darfur.

Maafisa huko Khartoum hivi karibuni wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kuelekea kura ya maoni ya Januari 9, ambayo huwenda ikapelekea Sudan Kusini kuwa taifa huru, lakini makundi makuu ya uasi huko Darfur bado yanapigana na majeshi ya serikali. Mapigano ya wiki za hivi karibuni yamesababisha zaidi ya watu 10,000 kukimbia nyumba zao.

Kura ya maoni ni sehemu ya mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza zaidi ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Sudan Kaskazini na Kusini.

Darfur imekumbwa na mgogoro tangu waasi waliponyenyua silaha mwaka 2003, wakiishutumu serikali kulitelekeza eneo la Sudan magharibi.
Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 300,000 wameuwawa katika mapigano huko Darfur na watu milioni 2.7 wengine walikoseshwa makazi. Serikali ya Sudan imetoa idadi ya chini ya vifo katika eneo hilo, kuwa ni watu 10,000 waliokufa.

XS
SM
MD
LG